Gilberti wa Sempringham

Mt. Gilberti.

Gilberti wa Sempringham (Sempringham, karibu na Bourne, Uingereza, 1083 hivi -Sempringham, 4 Februari 1189) alikuwa padri halafu abati wa shirika la kimonaki alilolianzisha kwa idhini ya Papa Eujeni III, la pekee kuanzishwa nchini, likiwa na waklero waliofuata kanuni ya Mt. Augustino na wanawake waliofuata ile ya Mt. Benedikto [1].

Alitangazwa na Papa Inosenti III kuwa mtakatifu tarehe 11 Februari 1202.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Februari[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/39550
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy